MCHUNGUZI MKUU TAKUKURU AMWANDIKIA BARUA DPP KUKIRI MAKOSA YAKE


Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyika (44) anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo kushawishi rushwa ya zaidi ya Sh. milioni 300, kupokea na kutakatisha Dola za Marekani 20,000 amedai mahakamani amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya kukiri makosa yake.

Batanyika alitoa madai hayo jana kesi yake ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevini Mhina, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika.

Hata hivyo, mshtakiwa alidai kuwa amemwandikia barua DPP na kwenye makubaliano anasubiri majibu ndugu zake wanafuatilia.

Hakimu Mhina alisema kesi hiyo itatajwa tena Novemba 15, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post