JAFO AWATAKA WENYE MALALAMIKO YA KUONEWA KATIKA UCHAGUZI WAZIONE KAMATI ZA USULUHISHI

Na Joctan Augustino, APC BLOG NJOMBE 

Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo ameagiza  mtu mwenye malalamiko ama dukuduku kuhusu mwenendo wa mchakato wa uchaguzi kuwasilisha pingamizi katika kamati zilizoundwa kwa mujibu wa sheria nchi nzima ili kupatiwa ufumbuzi wa malalamiko yao.

Waziri huyo amesema kamati hizo zimejumuisha wajumbe ambao hawatoki kwenye mamlaka za kiserikali ili ziweze kufanya kazi bila kuingiliwa na chama ama mtu yeyote mwenye mamlaka kwa lengo la kutatua malalamiko na dukuduku za wananchi kwa maslahi ya taifa katika kipindi chake chote cha kazi kuanzia nov 5 hadi nov 9.


Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Njombe,kikosi cha kamati ya muda ya rufani iliyoundwa pamoja kamati za ulinzi na usalama wilaya waziri jafo amesema amelazimika kuunda kikosi hicho ili kuhakikisha haki inatendeka katika kuwapata viongozi sahihi watakao aminika na kuchaguliwa na wananchi ifikapo nov 24 na kuagiza kamati hiyo kuhakikisha inawarejesha wale wote waliotolewa kwa hujuma katika nafasi walizo gombea.

Awali akitoa tathmini ya kitaifa juu ya mchakato wa uchaguzi Jafo amesema katika mitaa 4200, vijiji 12 elfu na vitongpji elfu 64 ambayo ni sawa na asilimia 98.2 limekwenda vizuri huku akidai katika maeneo yenye asilimia 1.8 ambayo ni sawa na kata 72 kati ya 3956 lilikuwa na dosari na kuzitaka kamati rufani kwenda kuzitatua.


Baada ya kutangaza kamati hizo na kuzipa majukumu ya kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi ili kulinda haki za wananchi,watia nia na vyama vya siasa kisha akatoa onyo kwa wanasiasa wanaotoa matamko yanatolenga kuhatarisha amani ya nchi ambapo ameshauri kama kuna tatizo kuwasilisha katika kamati hiyo maalumu badala ya mitandaoni.


Nae mkuu wa mkoa wa Njombe akieleza mwenendo wa mchakato wa uchaguzi anasema katika mkoa wa Njombe hali ni shwari kwasababu hakuna malalamiko amabayo yametolewa na vyama vya siasa huku akieleza kwamba vyama vilivyojitokeza katika kinyang'anyilo kuwa ni CCM ambayo imechukua na kurejesha fomu 9679,Chadema zikiwan 1498,ACT fom 1 pamoja na cuf yenye fomu 14.

Katika mchakato wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wa serikali za mitaa watanzania wamehimizwa kuendelea kudumisha amani na kuepukana na shali ambazo zinaweza kuharibu sifa ya taifa letu

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post