EBITOKE AMVAMIA MLELA NA MPENZI WAKE KWA FUJO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI


Mchekeshaji Ebitoke ameuvamia mkutano wa Mwigizaji Yusuph Mlela na Waandishi wa Habari Dar es salaam na kutaka kupigana na Mlela na Mpenzi wake mpya ambae alikua ameongozana nae kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari ikiwa ni siku chache tu toka Mlela adaiwe kuachana na Ebitoke.

Ebitoke amesikika akisema; “Mwacheni nimwonyeshe”, huku akitukana matusi ya nguoni licha ya kudhibitwa na mabaunsa.


Kaka wa Ebitoke naye amesikika akimwambia Mlela, “Umemuharibia maisha mdogo wangu” huku waandishi wa habari na wasanii wenzake waliokuwepo wakibaki wameduwaa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post