"WAPINZANI NI WADUDU" ASEMA MBUNGE WA CHAMA TAWALA TANZANIA


Mbunge wa chama tawala nchini Tanzania, Rashidi Chuachua wa jimbo la masasi mjini amewataka wananchi wa jimbo hilo kutowachagua viongozi wa vyama vya upinzani kwa kuwa hao ni wadudu.
 

"Sisi kama CCM hatupo tayari kufanya kazi na wadudu, msituletee wadudu. Na hii wairekodi, mimi nawaita wadudu. Tunataka kufanya kazi na watu ambao wako tayari kujenga nchi na sio majungu na midomo," alisema mbunge Chuachua.

Kauli hiyo ambayo imezua gumzo katika mtandao na kufananishwa na kile kilichotokea katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwa sababu kuna watu waliokuwa wanawaita wenzao mende.
Hivyo kutafsiriwa kama uchochezi.

Wanasheria maarufu nchini humo, Fatuma Karume na Jebra Kambole wamevuta mjadala mkali kutoka kwa watu ambao wanahoji , wadudu ina maana gani?

Katika mjadala huo, wengine wanahoji kuhusu hao wanaopiga makofi kwa kumshangilia, je kile wanachopigia makofi wanafurahishwa nacho au hawakuelewa maana yake.
 
Mchambuzi wa masuala ya siasa Mohamed Issa, anasema kuwa nafasi ya mbunge katika jamii ni kubwa sana na lugha ambazo kiongozi huyo anatumia zinaweza kumfanya akose nafasi ya ushindi.
"Hafai kuwa kiongozi, lugha ndio dhamana ya kiongozi" amesema Mohamed Issa.

Aliongeza kusema kuwa "Hizo sio lugha za kusikika kutoka kwa viongozi,
Kile kilichotokea nchi ya jirani ya Rwanda ni mafunzo tosha". Mohamed Issa alisisitiza.

Kauli hiyo ya wapinzani kuitwa wadudu imetamka wakati ambao wananchi wa taifa hilo wamekuwa na muitikio mdogo wa kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24.
 
Aidha mbunge huyo alitoa ufafanuzi wa kauli yake.
"Hiyo itakuwa tafsiri zao tu. Mimi ni mwanasiasa nimetamka nikiwa kazini. Nimesema binadamu kamili ana utashi, issue yangu ni kwamba kila mtu anaona tunachofanya. Mwenye utashi anaweza kufafanua, akakosoa," Chuachua aliliambia gazeti la Mwanachi jana.

"Asiye na utashi hawezi kuona zuri wala baya. Hata mdudu hajui zuri wala baya. Kwa hiyo watu wanaweza kutumia tafsiri hii kwa namna wanavyotaka wao".

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post