WAKAZI KATA YA RAMADHAN WAMSAIDIA MKANDARASI KUSOGEZA UMEME MAJUMBANI MWAO

Na Joctan Agustino, Njombe

Wakazi wa mtaa wa Itulike kata ya Ramadhani halmashauri ya mji wa Njombe wameshindwa kuzuia hisia zao na kuamua kushiriki katika zoezi la uchimbaji mashimo ya kusimika nguzo za umeme pamoja na kusafisha njia za kupitisha nguzo za umeme ili kuharakisha zoezi la usogezaji wa huduma hiyo ambayo hawajaipata tangu uhuru licha ya mtaa wao kuwepo katika kata ya mjini.


Wakazi hao akiwemo  Michael Jacob ambaye ni mkiti wa mtaa  pamoja na Angela Exavel  wanasema wamelazimika kushirikiana na jopo la mafundi wa Tanesco kusogeza vifaa vya ujenzi wa mradi, uchimbaji wa mashimo ya nguzo pamoja na usafishaji wa njia za umeme ili kuipunguzia mzigo mafundi umeme ambao wamefika kwa ajili ya kukamilisha zoezi la uunganishaji wa nishati hiyo.

Wanasema ujio wa nishati ya umeme katika eneo hilo utaharakisha maendeleo kwasababu kwa kipindi kirefu wamekuwa wakifata umbali wa zaidi ya km 10 hadi 15  mashine za mafuta kusaga huku pia viwanda kadhaa kikiwemo cha maziwa vikishindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na ukosefu wa huduma ya umeme

Ujio wa timu ya mafundi iliyoweka kambi mtaa wa Itulike ikiongozwa na Naftali Kiula ambaye ni mkandarasi kutoka kampuni tanzu ya tanesco ya Electrical Transmision and Distribution Company ITDCO unawafanya wananchi kuhoji ukombo wa utekelezaji wa mradi huo jambo ambalo linatolewa ufafanuzi na mkandarasi.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa nae katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe ameshiriki katika uchimbaji wa mashimbo ya kusimika nguzo anasema wamepata shida kwa kipindi kirefu ya kufata huduma umeme vijiji jirani wakiwa na mizigo kichwani na kwamba ujio wa nishati hiyo utachagiza maendeleo katika eneo hilo linalotambulika kama bustani ya tunda la parachichi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post