WAANDISHI ARUSHA PRESS CLUB WAHITIMU MAFUNZO YA VIDEO GRAPHICS, WAASWA

Mwenyekiti wa Chama cha waendesha utalii Tanzania (TATO), Willy Chambulo katikati aliyevaa joho la njano na kofia nyekundu akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi kuhusu Video Graphic ambao ni wanachama wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha (APC)

Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu akizungumza katika graduation ya kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kuhusu Video Graphics yaliyokuwa yakitolewa katika chuo cha mafunzo ya uandishi wa habari cha Habari Leo

Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya APC, Jane Edward akimkabidhi Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo zawadi ya cheti cha heshima kwa ushirikiano wake ambao amekuwa akiutoa kwa chama cha waandishi wa habari APC ikiwa ni pamoja na kufanikisha kufanyika kwa mafunzo hayo

Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo akihutubia wahitimu wa mafunzo ya video graph (hawapo pichani), akisisitiza matumizi sahihi ya elimu waliyoipata na kuahidi kuendelea kusaidia waandishi wa habari kupata mafunzo zaidi.

Wahitimu wa mafunzo ya Video Graphic wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TATO Willy Chambulo  wa pili kutoka kushoto waliosimama mbele pamoja na viongozi wa chuo cha uandishi wa habari na uongozi cha Habari Maalum Media

Na Seif Mangwangi, Arusha

WAANDISHI wa habari pamoja na wapiga picha za mnato wametakiwa kubadilisha mtindo wa ufanyajikazi wa shughuli zao na kuwa za kibiashara Zaidi ili kujipatia kipato kikubwa tofauti na hivi sasa.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha waendesha utalii nchini (TATO), na Mmiliki wa kampuni ya Kibo guides Willy Chambulo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya muda mfupi kuhusu utengenezaji wa video (Video graphic), yaliyokuwa yakitolewa katika chuo cha uandishi wa habari cha Habari Maalum.

Chambulo amesema kutokana na mabadiliko ya kasi ya kiteknolojia waandishi wahabari wanapaswa na wao kubadilika na kuaandaa habari zenye ubora wa hali ya juu ili kuwavutia watazamaji.

Amesema kila mara atakuwa tayari kusaidia waandishi ambao watakuwa tayari kujiendeleza kielimu ili kuweza kuwajengea uwezo katika utendaji wao wa kazi wa kila siku kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.

“Binafsi niko tayari kusaidia makundi mengine ya waandishi wa habari waje hapa wapate elimu hii ambayo nina uhakika itawasaidia sana kwenye utendaji wenu wa kazi wa kila siku hasa katika kutangaza utalii wetu,”anasema.

Anasema amefurahishwa sana na hatua ambayo Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), kupeleka wanachama wake kujifunza mafunzo hayo na kuahidi kulipia kundi lingine la waandishi wa habari ili wapate elimu hiyo.

Awali akitoa risala ya wahitimu hao, Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu amesema mafunzo hayo yatawawezesha kuboresha kazi zao za kila siku kama wanahabari kutokana na umuhimu wake katika utendaji wa kazi za kihabari.

Amesema kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ambapo dunia hivi sasa imekuwa ikielekea katika masuala ya kidijitali, mafunzo ya uhariri wa habari za kidigitali ni muhimu kwa kila mwandishi wa habari ili aweze kukabiliana na mabadiliko hayo.

Mafunzo hayo ya mwezi mmoja na ambayo yanatarajiwa kuanza kwa mara nyingine hivi karibuni yametolewa kwa waandishi wa habari kumi pamoja na wapiga picha za mnato kumi na yamekuwa yakitolewa kwa mfumo maalum ambao umeanzishwa na uongozi wa chuo cha uandishi wa habari cha Habari Maalum.

Waandishi wa habari waliohitimu mafunzo hayo ni pamoja na Abraham Gwandu, Cynthia Mwilolezi, Mustafa Leu, Lilian Joel, Janeth Mushi, Allan Isack, Claud Gwandu, Veronica Ignatus, Deo Moita na Jane Edward.

1 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

  1. Mafunzo mazuri sana elimu haina mwisho ,hungereni sana Wahenga kwa hatua hiyo muliyofokia mumekuwa ni taa kwa wengine watakaofuatia mwanzo mzuri

    ReplyDelete
Previous Post Next Post