SIMBA YAWATWANGA MASHUJAA NYUMBANI


Bao pekee la Simba SC kupitia kwa Sharaf Shiboub mnamo dakika ya 56 kipindi cha pili, limeipa ushindi timu hiyo dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mashujaa FC uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Simba imecheza mechi yake ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu Bara msimu huu.

Katika mchezo huo, uwanja wa Lake Tanganyika ulionekana kuwa na changamoto haswa kwa Simba kutokana na vipara vingi na sehemu kadhaa zikiwa hazina nyasi.

Mapema baada ya mechi kumalizika, Beki Yusuph Mlipili, amesema wangeweza kushinda zaidi ya bao tatu lakini uwanja ulikuwa shida kwao.


"Uwanja kwakweli upande wetu ulikuwa na changamoto nyingi.


"Tungeweza kushinda zaidi ya bao tatu, hii imepelekea tushindwe kucheza kama ambavyo tumezeoa kucheza siku zote," amesema Mlipili.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post