MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKILIZA KESI 60 KWA NJIA YA MTANDAO


Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mhe. Richard Mziray akisikiliza kesi kwa   njia ya mtandao   “Video Coference”.
Mleta maombi Victor Binamungu (katikati) akiendelea na kesi yake dhidi ya Farida Hamza (kulia) na Geofrey Kabala (kushoto).
Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania, Mhe. Shabani Lila akiendesha kesi kwa mfumo huo (kushoto) Wakili Dkt.  Masumbuko Lamwai.
Edward Chuwa na Aaron Kabunga wakifuatilia kesi baina yao wakiwa mkoani Mwanza.
(Picha na Mary Gwera – Mahakama)


Na Magreth Kinabo – Mahakama

Mahakama ya Rufani Tanzania inatarajia kusikiliza jumla ya kesi 60 kwa kutumia mfumo wa mawasiliano kwa njia ya picha maarufu jina la ‘Video Conference’ kuanzia Oktoba 9 hadi 16, mwaka huu.

Mfumo huo ambao husaidia Mahakama ya Tanzania kuokoa fedha zinazotumika kuendesha kesi mbalimbali na muda unaotumika, ikiwemo kuwapunguzia gharama wanazozitumia wananchi kufika mahakamani kwa ajili ya kutafuta haki zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Elizabeth Mkwizu, Mahakama hiyo itasikiliza kesi madai na jinai, zilizoko katika Masjala ya Tabora, Mwanza, Bukoba na Mbeya, ambazo zitasikilizwa na Majaji tofauti 17 wa Mahakama ya Rufaa.

Hivyo Mahakama hiyo, imeanza kusikiliza kesi hizo mapema Oktoba 9, mwaka huu na imesi
kiliza jumla ya kesi 12, zilizoko katika masjala ya Mwanza na Tabora kwa kutumia mfumo huo.

Kwa upande wa Mwanza, Mahakama hiyo imesikiliza kesi sita, kati ya hizo mbili zimesikilizwa na Mhe. Jaji Stella Mugasha, katika Kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Jaji Mugasha alisikiliza kesi  ya maombi namba 447/08/2019  ya Benjamin Manota na wenzake ambao ni Mwana Selemani na Mussa  Benjamin dhidi ya Geita Gold Mine Limited, ‘The Principal  Secretary Minisrty of Minerals’ na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi hiyo imeahirishwa kwa sababu wadawa wote wamefariki mpaka watakapochaguliwa wasimamizi wa mirathi.
Kesi ya pili kusikilizwa na Jaji huyo ni kesi ya maombi ya madai namba 31/08/2019 ya Tella Bupamba dhidi ya Elisha Shija, inayohusu kuomba kuongezewa muda wa kibali cha kuja Mahakama ya Rufaa na imesikilizwa pande zote mbili na yanasubiriwa maamuzi yakiwa tayari wahusika watajulishwa.
Mahakama hiyo pia imeskiliza kesi ya tatu ambayo imesikilizwa na Mhe, Jaji Richard Mziray. Kesi hiyo namba 46/08/2019 ya Samwel Munsiro dhidi ya Chacha Mwikwabe.
Katika kesi hiyo Samwel ameomba nyongeza ya muda kuwasilisha kibali Mahakama Kuu ili aweze kuwasilisha maombi ya mara ya pili baada maombi ya awali kukataliwa, ambapo Mwikwabe alidai kuwa maombi yake hayana mantiki.
Mhe. Jaji Mziray alisema amewasikiliza na kuangalia nyaraka, hivyo atatoa uamuzi na utakapokuwa tayari watapewa.

Jaji Mziray pia alisikiliza kesi ya madai ya maombi namba 602/08/2017 ya Victor Binamungu dhidi ya Geofrey Kabala na Farida Hamza.

Kesi hiyo ilihairishwa ili kutoa nafasi kwa Farida kuwasilisha nyaraka ya maelezo ya kesi na Majibu ya kiapo cha mleta maombi na kuhakikisha Victor na Geofrey wamezipata ndani ya siku 14 kuanzia Oktoba 9 mwaka huu. 

Kesi ya tano kusikilizwa ni madai ya maombi namba 63/17/2018 inayomhusu ‘The board of trustees of the National Social Security Fund,’ iliyowakilishwa na Wakili Dkt. Masumbuko Lamwai dhidi ya Nakara Hotel Limited, aliyewakilishwa na Dkt. Tugemeleza Nshalla, imesikilizwa na Mhe. Jaji Shabani Lila.

Jaji Lila aliahairisha kesi hii kwa sababu Dkt. Nshalla anaumwa, hivyo itasikilizwa siku nyingine.

Kesi nyingine ya sita ya madai namba 32/08/2019 ya Edward Chuwa dhidi ya Aaron Kabunga, ambapo Chuwa aliomba kuongezewa muda.

Akisikiliza kesi hiyo Jaji Lila alisema hayana msingi katika Mahakama hiyo na alimwamuru mleta maombi kumlipa gharama aliziotumia mjibu maombi. 

Kwa upande wa masjala ya Tabora kesi sita zimesikilizwa, ambazo ni ya madai moja na jinai tano.Kesi hizi zimesikilizwa na majaji mbalimbali katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Kesi zilizosikilizwa ni ya jinai namba 03/20/2015 ya Juma Kahukule dhidi ya Jamhuri,jinai namba 2/ ‘B’/2015 ya Hamis Mashishanga dhidi ya Jamhuri, jinai namba 3/20/2016 ya Chiganga Mapesa dhidi ya Jamhuri namadai namba 524/11/2018 ya Athumani Mauruti dhidi ya Yusta Maganga.

Nyingine ni jinai namba 02/2016 ya Hussein Masoud dhidi ya Yusuph Said na jinai namba 4/2016 ya Yusuph Said dhidi ya Jamhuri.

Kesi nyingine zitasikilizwa kwa kutumia mfumo huo, Oktoba 10, 15 na 16 mwaka huu. Mfumo huo ulianza kutumika rasmi Desemba 5, mwaka 2018, ambapo Mahakama ya Tanzania ilianza kutumia vitendea kazi vyake yenyewe.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post