WANASHERIA CHIPUKIZI WATAKIWA KWENDA KUFANYA KAZI VIJIJINIJaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mohammed Othman Chande akitoa Lecture kwa wanasheria wachanga kuhusu majukumu yao kwa jamii na taaluma hiyo wakati wa sherehe ya majadiliano baina ya wanafunzi hao iliyofanyika katika chuo cha sheria jijini Dar es Salaam.
Balozi Juma Mwapachu akizungumza na wanasheria wachanga wakati wa sherehe ya majadiliano baina ya wanafunzi wa sheria, iliyofanyika mijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (TDHRC), Onesma Olengurumwa akizungumza wakati wa sherehe ya majadiliano baina ya wanafunzi hao iliyofanyika katika chuo cha sheria jijini Dar.
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO

JAJI Mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania, Mohamed Chande Othman amewataka mawakili watarajiwa kwenda kufanya kazi vijijini kama maofisa wa mahakama wakasaidie katika utoaji haki kwani asilimia 70 za kesi nchini zipo Mahakama za Mwanzo lakini wananchi wanajiwakilisha wenyewe.

Jaji Chande ameyasema hayo wakati akitoa mhadhara (Lecture) wa Jukumu la wanasheria chipukizi kwa umma na mwelekeo wa sekta ya sheria Tanzania kwa wanasheria wachanga jijini Dar es Salaam walipokutana pamoja kujadiliana mambo mbali mbali ikiwemo kuhamasisha wanasheria wachanga ambao bado hawajasajiliwa na wale waliosajiliwa kufanya kazi kwa weledi.

Amewaambia kuwa wakiwa kama wanasheria vijana wanapaswa kuhakikisha wanafikia wananchi waliopo vijijini ili kuwasaidia katika masuala yao ya kisheria na kusaidia mahakama katika utoaji haki kwa haraka zaidi kwani mawakili wengi wamekuwa wakiishia kufanya kazi mijini kuliko vijijini.

Pia amewataka kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuafuata maadili yao kwa kuwa wakweli na kuepuka vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanalinda utawala wa sheria na haki za msingi, uhuru na wajibu.

“Katika Mkoa wa Lindi, kuna wakili mmoja huku mawakili nane wakiwa katika Mkoa wa Katavi, 20 mkoani Ruvuma, 29 Kigoma na 38 wapo mkoani Mara.

Aidha Jaji Chande amesema kuna baadhi ya mikoa takribani saba ya Tanzania Bara haina Mahakama Kuu kama vile, Lindi, Katavi, Morogoro, Simiyu, Manyara, Pwani, Singida and Songwe huku Wilaya 28 zikiwa hazina Mahakama za Wilaya kama vile Mkinga.

“Kutokuwepo kwa mahakama ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa haki na masuala ya sheria hususani kwa mawakili wachanga. Hivyo, tutaendelea kuishauri serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili watu waweze kupata haki zao natambua kuna mchakato wa mahakama wa kuhakikisha kila wilaya inakuwa na mahakama,” amesema Jaji Chande.

Amefafanua kuwa katika ripoti ya dunia ya mwaka 2019 kuhusu utoaji haki inaonesha watu milioni 230 wanaoishi katika mazingira mbalimbali wanakosa haki huku watu bilioni 1.5 wanashindwa kutatua matatizo yanayowakabili yanayohusu haki na watu bilioni 4.5 wametengwa na fursa zitolewazo na sheria na inaonesha kutokuwepo kwa usawa au ufikishaji sawa wa haki kwa wote na ukosefu mkubwa wa uwakilishi wa kisheria.

Jaji Chande amesema katika miaka mitano iliyopita zaidi ya asilimia 50 ya mawakili wamepokelewa nchini kufanya kazi hivyo, anaamini wataendelea kubadilisha muundo na taasisi ya sheria.

Kwa upande wake Balozi Juma Mwapachu amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika kuimarisha miundombinu ya mahakama lakini bado watu wengi wana uhitaji wa kusaidiwa katika masuala ya utoaji haki.

“Wanasheria wachanga wanatakiwa kujua wanaisaidiaje jamii katika masuala ya sheria pamoja na kupigania haki za binadamu, uhuru wa kuongea na katiba” amesema.

Naye, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu (TDHRC), Onesmo Olengurumwa amesema ni wakati wa mawakili kuhakikisha wanakwenda vijijini kuwasaidia wananchi waliowengi ambao hawajui masuala ya sheria.

Amesema, wanasheria wanapaswa kuwa na wito na uelewa mkubwa katika kuendesha kesi zenye maslahi kwa umma na zile za ki mkakati zaidi.

Olengurumwa ameongeza kuwa, kwa sasa kuna changamoto kubwa kwa mawakili kurundikana mijini, kwani nchini kuna mawakili wapatao 8000 lakini nusu ya hao wako mijini hivyo wanapaswa kujua wameitwa katika kazi hivyo kusaidia watu wote.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post