SOKA: Tanzania yajiweka katika mazingira magumu kufuzu Fainali za (CHAN)

Image result for taifa stars chan
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kilichofungwa na Sudan 1 - 0 katika harakati za kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani mwakani nchini Cameroon

Tanzania imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani nchini Cameroon baada ya kufungwa 1-0 nyumbani jana na Sudan katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili na ya mwisho ya mchujo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

 Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, bao lililoizamisha Tanzania limefungwa na Yasir Mozamil dakika ya 60 akimalizia mpira uliourudi baada ya kugonga mwamba kufuatia krosi ya Ranadan Agab aliyefanikiwa kumtoka beki wa kulia, Boniphace Maganga. 

Sasa Tanzania wanatakiwa kwenda kushinda 2-0 ugenini kwenye mchezo wa marudiano ambao Sudan wameomba ufanyike mjini Kampala, Uganda Oktoba 18 kwa sababu ya machafuko yanayoendelea nchini mwao.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post