MWANDISHI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUCHAPISHA HABARI YA UONGO FACEBOOK ,APELEKWA MAHABUSUMwandishi wa  habari wa kujitegemea   anayeandika  habari  zake  katika ukurasa  wa kitabu sura (face Book )katika  wilaya ya Mufindi  mkoa wa  Iringa  Sebastian Atilio  amefikishwa  mbele ya  hakimu  mkazi  wa mahakama ya   wilaya ya  Mufindi kwa  makosa mawili  likiwemo la kuandika habari za uongo na  kufanya kazi  bila  kusajiliwa na bodi  anaripoti mwandishi Francis Godwin kutoka mkoani Iringa .

Akisoma  mashtaka  haya  leo   mbele ya hakimu  mkazi wa mahakama  hiyo  Edward  Uforo, mwendesha mashitaka wa jamhuri Victor  Kitamale  alisema  kuwa  Sebastian  anashtakiwa  kwa  kosa la kwanza la kufanya kazi  bila  kusajiliwa  katika  bodi ya  uandishi na  kosa la  pili ni  kuandika habari za uongo  juu ya  wananchi wa  kijiji cha Ifupila  kuhamishwa .
Hata   hivyo msitakiwa   huyo alikana mashitaka  yote yanayomkabili  huku  mahakama  hiyo  ikisema  kuwa makosa  hayo  kisheria  yanadhamana  .
Wakati  mwendesha  mashtaka  wa Jamhuri  alipinga  dhamana  hiyo chini ya  kifungu namba 148(5) D)  cha sheria  na mwenendo wa makosa ya jinai (sura 20) ambapo  jamhuri  imefaili  kiapo cha kuzuia dhamana  kutolewa .
Huku upande wa mashtaka  umepewa na mahakama hiyo    nafasi ya  kufaili hati  kinzani  Septemba 16  mwaka huu   ili Septemba  18  mwaka huu  maombi ya kutolewa ama  kutotolewa kwa dhamana  yatajulikana .
Wakili   wa mwanahabari  huyo Emmanuel  Chengula kutoka  mtandao wa  watetezi wa haki za binadamu (THRDC)  alisema kuwa  hatua ya kufikishwa mahakamani kwa mteja  wake ni mwanzo wa haki yake  kupatikana  kwani polisi  walikuwa  wakimzuia  mahabusu mteja  wao toka  jumamosi  iliyopita  bila  kumpeleka mahakamani.
 Wakili  Chengula  alisema  katika  kesi hiyo  kuna maombi ya  kuzuia  dhamana  ambayo ni  maombi namba 10/2019 na kesi  yenyewe   ya  msingi ni kesi  namba 208/2019.
Mshitakiwa   huyo amepelekwa katika mahabusu ya Isupilo  Mufindi hadi   septemba  18  atakapofikishwa  mahakamani hapo tena kwa ajili ya  kusikiliza maamuzi ya dhamana  yake.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post