ALIYEUA,KUKATA SEHEMU ZA SIRI ZA MCHUNGAJI NA KUPELEKA KWA SANGOMA AHUKUHUMIWA KUNYONGWA
Na Esther Macha - Malunde 1 blog Songwe 
MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya imemhukumu ,Amanirabi Kalinga (19) mkazi wa kijiji cha Mpanda wilayani Mbozi mkoani Songwe kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia kinyume na kifungu cha sheria 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 marekebisho ya sheria mwaka 2002.


Akitoa hukumu hiyo jana,jaji wa mahakama kuu kanda ya mbeyaDkt,Adam Mambi alisema mahakama imetoa hukumu hiyo kutokana na kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashitaka ambapo alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa vijana wengine wenye tabia za kujichukulia sheria mkononi.

Awali akisoma shauri hilo mahakamani hapo Jaji Mambi alisema mshitakiwa anakabiliwa na kesi ya kumuua na kisha kukata sehemu za siri za Heron Kalinga kisha viungo kupeleka kwa mganga wa kienyeji,mshitakiwa anakabiliwa na kesi namba 57 ya mwaka 2017.

Aidha Jaji Mambi aliongeza kuwa mshitakiwa alimkuta marehemu na wenzake wakichunga ng’ombe na kumchukua na kumpeleka kichakani na kumuua na kumtupa huku Joseph Mwashilindi akishuhudia, Heron Kalinga akiangushwa chini na kumchoma kisu ambapo baada ya tukio mshitakiwa alirudisha ng’ombe nyumbani kwa kina Heron Kalinga.

Alisema baada ya kufika nyumbani kwa marehemu alidai kuwa amewakuta wamepotea na baada ya kubanwa alienda kuonyesha mwili ulipo huku sehemu za siri za marehemu akiwa zimekatwa na alizipeleka kwa mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Makamu ambaye alihitaji viungo hivyo ili amfanyie dawa,(Ndagu).

Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasipo kuacha shaka,Kijana huyo atatumikia adhabu ya kunyongwa hadi kufa ili iwefundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama hizo.

Naye wakili wa Serikali, Shindani Michael alishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa wananchi wengine wenye nia ya kufanya makosa kama hayo ya kutaka kujipatia mali kwa kudhuru wengine.

Nje ya Mahakama,mamia ya watu waliofika mahakamani hapo kushuhudia hukumu hiyo,wakiongozwa na Yerode Samwel mkazi wa Mbozi,walisema mahakama hiyo imetenda haki kwa kuwa matukio hayo ya watu kuua wenzao ili wajipatie mali yamezidi kushika kasi.

Alisema hiyo itakuwa fundisho kwa wengine kwani vitendo vya baadhi ya watu kutaka utajili kwa kuua wenzao na kuchukua viungo kwa ajili ya kupeleka kwa waganga wa kienyeji vimekuwa vikijitokeza bila kujali kuwa ni kosa kisheria na ni dhambi mbele za Mungu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post